Tuesday, January 20, 2015

WAZIRI AWAOMBA RADHI WANAFUNZI KENYA

Waziri wa Usalama nchini Kenya, Joseph Nkaissery.
Waziri wa Usalama nchini Kenya Joseph Nkaissery amewaomba radhi wanafunzi wa shule ya msingi waliofyatuliwa gesi ya kutoa machozi wakati walipokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa kipande cha ardhi ambacho kilikuwa uwanja wao wa kuchezea.

Wanafunzi waliofyatuliwa gesi ya kutoa machozi kwa kuandamana kupinga unyakuzi wa uwanja wao.
Bwana Nkaissery amempa siku moja mnyakuzi wa ardhi hiyo kuondoa sehemu ya ukuta iliobaki baada ya wanafunzi kuuangusha na kisha kuondoka katika eneo hilo.


Nkaisery ameongeza kwamba serikali itaweka uzio katika ardhi hiyo na kuiacha kuwa uwanja wa kuchezea wa wanafunzi hao.

No comments:

Post a Comment