Kwenye moja ya mada ya zangu kuhusu vizuizi vya mafanikio ya
kimasomo tumeona suala la mwanafunzi kujihusisha na mapenzi limechukua nafasi
ya pili, hii ina maana kuwa wanafunzi wengi hupoteza mwelekeo wa kimasomo baada
ya kujiingiza katika ulimwengu wa mapenzi.
Jambo baya kabisa kwa wanafunzi ambao ni wenyeji wa masuala ya kimapenzi hivi sasa hasa wanawake ni kutokukumbuka namna walivyotekwa kimapenzi na wengi kati yao wanadai kuwa haukuwa utashi wao na kwamba walilazimishwa, aidha na watu, mazingira au misisimko ya miili, jambo ambalo si la kweli kisaikolojia.