Tuesday, January 20, 2015

AVUNJIKA TAYA, AOMBA MSAADA WA 60, 000/= ATIBIWE

Emmanuel Nelson akiwa wodini Hospitali ya  Taifa Muhimbili.
EMMANUEL NELSON mwenye umri wa miaka kati ya (30 au 35, ambaye ni  mzaliwa wa Mbamba Bay, Ruvuma, na ambaye wazazi wake wanaishi Dodoma, anaomba msaada wa kutibiwa taya ambalo limevunjika.

Nelson ambaye alishindwa kuongea akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alifikishwa na   polisi wa kituo kidogo cha Pangani, Ilala, jijini Dar es Salaam, Januari 15, mwaka huu baada ya kumwokota barabarani, anasemekana alivunjwa taya hilo kwa kupigwa na watu wasiojulikana.
Mtu huyo ambaye amelazwa katika wodi ya Sewa Haji namba 23, amesema ameshindwa kupata Sh. 60,000/= kwa ajili ya gharama za matibabu na kulazwa ambapo amesema ametelekezwa na ndugu zake wanaoishi Tabata-Relini, jijini Dar es Salaam.
Nelson anahitaji kufungwa waya na matibabu mengine ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida.
 Kwa  yeyote aliyeguswa na tukio la mgonjwa anaweza kumchangia kupitia namba ya simu 0655 207 156, pia anaomba ndugu, jamaa na marafiki wajitokeze kumwona na kumsaidia.

No comments:

Post a Comment