Tatizo la
wanafunzi wengi siku hizi wamekuwa na mtindo unaoitwa ‘copy and paste’ yaani
anachofundishwa ndicho wanachokishika na wakati mwingine kukiandika, jambo
ambalo huchagia kuwafanya wanafunzi washindwe kuwa ufahamu wa kutosha juu ya mambo
wanayoyasoma.
Katika hali
ya kawaida kazi kubwa ya mwalimu ni kumpa mwanafunzi moja kati ya mambo manne
yanayokamilisha pembe nne za kuta ya ufahamu.
Hii ina maana kwamba mwanafunzi anayepewa moja
na mwalimu hawezi kuwa imara kama yeye mwenyewe hakujenga kuta zake tatu za kujielewesha.
Haifai kuwa
mwanafunzi mwenye mfano wa kasuku, kuiga kilichofanywa na mwingine. Lazima
katika kila unachofundishwa uhakikishe kuwa unapata muda wa kukichambua kwa
kina na kuzidi kujielewesha zaidi ya pale alipoishia mwalimu.
Njia pekee
ya kufikia kiwango cha juu cha uelewa ni pamoja na kupata muda wa kuchambua na
kutafiti kile ulichofundishwa na kupata muda wa kuwashirikisha wengine kile
unachokijua zaidi ya ulichofundishwa darasani.
Mwanafunzi
ambaye atakuwa na tabia ya kuwaleza au kuwafundisha wenzake anachokijua zaidi
kuhusu jambo fulani ndiyo atakuwa anajijengea uwezo wa kufahamu zaidi na
kuimarisha kumbukumbu za kile alichofundishwa.
Kilio cha
wanafunzi wengi siku hizi ni usahaulifu.
Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa,
usahaulifu huo unatokana na tabia ya kukariri kama kasuku na kutokuwa na muda
wa kushirikiana na wenzake katika mijadala ya kujielemisha.
Nashauri
kila unachojifunza pata muda wa kukichambua kwa kina na pendelea zaidi
kuwafundisha na wengine juu ya kile ulichopata katika kujielimisha kwako.
Ukifanya hivyo utaongezeka kimaarifa kila siku na hutasahau ulichofundishwa. Wazungu
husema: "The miracle is this – the more we share, the more we have."
No comments:
Post a Comment