Friday, May 21, 2010

Hataki nimpigie simu usikuSWALI-Mimi ni msichana naishi Arusha, nilitokea kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kaka mmoja ambaye baadaye nilizaa naye mtoto mmoja. Tangu nijifungue nina miaka minne, kipindi hiki chote hatukuwa na mawasilino na mzazi mwenzangu. Hivi karibuni alijitokeza na kutaka turudishe uhusiano wetu nikakubali. Lakini amekuwa hataki niwasiliane naye wakati wa usiku na kuna kipindi nikimpigia simu anakata. Nilipojaribu kumuuliza hakunijibu zaidi ya kuwa mkali, nimweleweje?

JIBU-Mdogo wangu mambo mengi yanayotokea duniani yana dalili zake, mvua ikitaka kunyesha kwa mfano dalili zake huwa ni mawingu, malaria nayo ina dalili zake. Hata tunapozungumzia usaliti wa kimapenzi kuna dalili zake ambazo ni pamoja na hizo za mtu kutotaka kuwasiliana naye. Lakini, wataalamu wanasema dalili huwa si tatizo bali hutumika kutambua tatizo.

Kwa msingi huo, hatuwezi kumhukumu mpenzi wako kwa kutumia dalili za kutokuwa mwaminifu, nakushauri uwe makini naye na umchunguze kwa nini hataki kuwasiliana nawe. Ikiwezekana akupeleke nyumbani kwake na akupe uhuru wa kufika huko kama mzazi mwenzake wakati wowote. Lakini pia ni vema ukamuuliza kulikoni akuzuie jambo jema kama hilo la mawasiliano tena nyakati ambazo ni za kuliwazana? Maana mchana ndiyo watu huwa bize sasa usiku kulikoni? UKIMWI UNAUA!

1 comment:

  1. SIKU ZOTE ZA MAISHA YA BINADAMU MTAKA MAWILI MOJA HUMPONYOKA HAPA KWA JINSI NILIVYOISOMA HABARI HII HUYU MZAZI MWENZAKO DADA AMEISHA PATA MKE MWINGINE NA HUWEZEKANA KABISA KIPINDI ANAKUJA KWAKO ILI MUWEZE KUSTAREHE KIMAPENZI NI BAADA YA KUONA AIDHA MKE WAKE MWINGINE ANA UDHURU WA KITU FULANI BASI YY NDIPO HUTUMIA MWANYA HUO KUJA KWAKO KI UKWELI HUYO JAMAA ACHANA NAE KWANI ANAWEZA KUKULETEA UKIMWI NA HAKUNA KITU CHA THAMANI KAMA UHAI, MUNGU ATAKUPA MUME MWEMA NA UTAMFURAHIA TU.NA KISA ANACHOKATAA KWAMBA USIMPIGIE SIMU KWANI ATAKUWA KAMDANGANYA HUYO MKE WAKE MWINGINE KUWA HANA MPENZI WALA MKE NDIO MAANA UKIPIGA SIMU UNAWEZA UKAMHARIBIA KWA HUYO ALIYENAYE SASA.

    ReplyDelete