Friday, April 9, 2010

WASICHANA WANAFUNZI WANANICHANGANYA
SWALI.......Anko mimi ni mvulana miaka 20, nafanya kazi. Tatizo ambalo nakabiliwa nalo ni kuwapenda wasichana ambao ni wanafunzi. Nasema hili ni tatizo kwa sababu hisia zangu za mapenzi haziko kwa wasichana wa kawaida mtaani. Mimi Anko nikiwaona wasichana hasa wakiwa na sare yaani nachanganyikiwa kabisa. Naomba ushauri wako.


JIBU........Ushauri wangu wa kwanza ni kwamba acha kufanya mapenzi na wanafunzi ni hatari na hasa wale wenye umri mdogo kwani ikibainika adhabu yake ni kifungo cha miaka 30 jela.

Kuhusu kuchasnganyikiwa unapowaona, hili ni tatizo la kisaikolojia ambalo linatokana na kinasa hisia chako kulewa aidha udanganyifu kutoka kwa watu wako wa karibu au maumbile yao kukuvutia.Hapa ingekuwa vema kama ungepata muda unione ili nizungumze nawe uniambie, ili mwanamke akuvutie awe na sifa gain? Maana inawezekana kinachovuta hisia zako ni ‘matiti saa sita’ na sura za kitoto, hivyo huwezi kuwapenda wasichana ambao hawana sifa hizo mpaka utibiwe athari hiyo ya kisaikolojia.

Lakini pia inawezekana katika makuzi yako, ulidanganywa na watu kuwa wasichana wadogo ni bora kimapenzi kuliko watu wazima na wewe ukaamini hivyo, ndiyo maana leo ukiwapata wa saizi yako hawakusisimui. Unachoweza kufanya katika hatua za mwanzo ni kuwa na ufahamu utakaokutia hofu. Katika hali ya kawaida watu hawanywi sumu kwa sababu wanaogopa kufa, hawashiki moto kwa wanaogopa kuungua.

Siku zote hofu hujenga tabia njema, itafute hofu ya kuchezea wanafunzi kwa kufikiria kuwa ukiwa nao siku moja watakutia gerezani na utaozea huko. Ukiipata hofu hiyo, bila shaka hutawatamani kabisa.

Kuhusu kushindwa kuwapenda wa saizi yako hilo ni tatizo la mazoea, ambao unaweza kuyajenga kwa kujilazimisha, huku ukiondoa vitu mbadala. Ili mtu apende kiazi lazima umuondolee mkate na siagi na wewe ukiwandoa wanafunzi akilini mwako utawapenda wa saizi yako bila shaka.

No comments:

Post a Comment