Friday, April 9, 2010

NATAFUTA NJIA YA KUACHANA NAYE
SWALI.......Swali langu kwa Mshauri ni kwamba, mimi ni msichana ambaye nina mpenzi wangu niliyempa moyo wangu wote kwa kumwamini kuwa atakuwa mume wa maisha yangu. Lakini siku za hivi karibuni amebadilika, mara nyingi nimefuma meseji za mapenzi kwenye simu yake na wakati mwingine nimemuona laivu. Naumia sana lakini nashindwa kumuacha kwa sababu nampenda, mshauri nisaidie njia ya kumwacha mwanaume huyu ataniua bure.JIBU........Kitaalamu mwanzo wa mapenzi huwa ni rahisi kuliko mwisho wake. Hii inatokana na ukweli kwamba mapenzi ni sawa na ulevi ambao mtu akiuzoea ni vigumu kuuacha kwa mara moja, ndiyo maana tunaona watu wanateswa lakini wanashindwa kuamua kuachana na wapenzi wao kwa sababu kama hizo zako. Sasa ili mtu afikie uamuzi wa kuachana na mtu aliyekuwa naye kama mpenzi kwa miaka mingi lazima ajue kanuni, vinginevyo moyo hautakubali.

No comments:

Post a Comment