Tuesday, April 13, 2010

Q, JAY APATA JIKOBaada ya kukukuruka kwa muda mrefu, hatimaye Msanii mkali wa R&B nchini anayejulikana kwa jina la Q. Jay hivi karibuni Amani Usiamini ilinyaka ishu kwamba mshikaji ameamua kumuoa demu mmoja aitwaye Elizabeth na kwamba ndoa hiyo ilifungwa kwenye kanisa la St. Peter jijini Dar es Salaam Aprili 10, habari hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Dj Choka.

Amani usiamini huu ni uamuzi mzuri alioufanya dogo, kwani suala la wasanii kuoa limekuwa gumu kimtindo. Hata hivyo safu hii inatangulizia salama kwamba kuoa peke yake si ishu kiiivyo bali kudumu na uliyeoana naye ni mfupa unaowashinda mastaa kibao.

No comments:

Post a Comment