Tuesday, April 13, 2010

MANENO MANNE MUHIMU KWA PENZI LA MWANAMKE




Imebainika kwamba, wanaume wanaposaka wapenzi, huwa tayari kutii masharti wanayopewa na upande wa pili. Utii huu ndiyo unaotajwa kumvutia mwanawake kiasi cha kumfanya aamini kirahisi kuwa mwanaume wa maisha yake ni huyo anayemtongoza wakati huo.

Hakuna shaka kwamba, katika mazungumzo ya awali ya mwanaume anayemteka mwanamke kimahaba, kinywa chake huwa hakikauki maneno haya manne zenye nguvu ya kumdatisha mwanamke, ambazo ni NAKUPENDA, NAKUHITAJI, SAMAHANI na ASANTE.

Ni wazi kwamba kuna wanaume wengi ambao huanza na gia kubwa ya maneno hao wamebainika kupoteza mvuto wa kimapenzi waliokuwa nao mwanzo kwa wapenzi wao. Binafsi nathibitisha hili kwa kuwa nimeshafanya uchunguzi kupitia wanaume wanaonijia kutaka majibu ya kwa nini wapenzi wao wamewageuka na kutokuwapenda kama awali.

Kabla ya kuwashauri nimekuwa nawadodosa na hatimaye kutambua kuwa waliacha kutumia maneno hayo mara tu walipoona amefanikiwa walichokuwa wanakitafuta.
Kama nilivyosema neno la kwanza lenye nguvu ya kumteka kimapenzi mwanamke ni NAKUPENDA. Neno hili ni tiba inayoponya hofu na kumfanya mwanamke ajiamini.
Neno la pili, NAKUHITAJI. Kama inavyokuwa wakati wa kutongoza, mwanamke anapenda kuambiwa neno hilo na kufanyiwa vitendo inavyoonesha kuhitajika kwake katika maamuzi, matembezi, faraja na muongozo wa kimaisha. Sambamba na hilo mwanamke anapenda sana kupewa ASANTE katika yale anayofanya.

Jambo la mwisho kabisa ni SAMAHANI. Ndugu zangu kuna wanaume ambao hawako tayari kuomba msamaha kabisa hata kama wamekosa kosa kubwa na la wazi kiasi gani? Kifupi tabia hiyo haipendezi. Ni busara kwa mwanaume kumuomba radhi mpenzi wake, ili naye ajione ni mwenye mamlaka na hivyo kuzidisha upendo na uangalizi wa tabia mbaya za mwanaume.
Niishie hapa kwa kuwashauri wanaume kuwa wakitaka kuwateka wanamke kimapenzi watumie kwa vitendo maneno haya manne. Kwa elimu zaidi ya mapenzi, ushauri wa kimasomo, saikolojia, habari na ucheshi tembelea blog yangu ya richmanyota.blogspot.com

No comments:

Post a Comment