Friday, April 9, 2010

2012 NDIYO MWISHO WA DUNIA



Tishio la kutokea mwisho wa dunia la Y2K lililotikisa mwaka 2000, limeibuka upya, baada ya taarifa kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya intaneti ulimwenguni kueneza habari kwamba Desemba 21 2012 ulimwengu utaangamia.

Dk. David Morrison, Mwanasayansi wa Shirika la NASA la Marekani amethibitisha kupokea barua pepe zaidi ya 1000, kutoka kwa watu waliotaka kujua kuhusiana na habari hizo.

Hakuna idara wala chombo cha kisayansi cha kuaminika kinachokaririwa katika taarifa hizo, lakini mitandao mingi ya intaneti imetia nguvu habari hiyo kiutabiri, huku imani za kidini zikihushishwa.

Inaelezwa katika habari hiyo kwamba, sayari moja ijulikanayo kwa jina la NIBIRU au Planet X itapoteza mwelekeo wake siku 4 kabla ya Sikukuu ya Krismasi mwaka huo na kuigonga dunia kisha kuisambaratisha.

Licha ya wanasayansi kupingana na hoja hiyo kwa madai kwamba mfumo wa sayari hauna tishio hilo, watoa taarifa wamezidi kusema kwamba, wanachoamini kimetabiriwa pia na mtabiri maarufu Nostradamus.

Nostradamus anatajwa kutabiri matukio mengi likiwemo la Marekani kushambuliwa na magaidi (Septemba 11), kutawaliwa na Rais mweusi, Barack Obama , mambo ambayo yote yametimia.

Mbali na utabiri huo, wapembuzi wa maandiko matakatifu ndani ya Biblia nao wametajwa kuhusisha mwaka 2012 na vita ya Armageddon itakayokuwa baina ya watu wema na waovu ambapo Kitabu cha Ufunuo kinaeleza yatatokea maafa ya kutisha.

Aidha, kalenda ya kabila la Mayan lililoko Amerika ya Kati, ambayo inaamika katika utabiri wa matukio, imetajwa na watoa habari kwamba dunia itafikia kikomo Desemba 21, huku volcano ya mawe ya njano ambayo hutokea kila baada ya miaka 650,000 nchini Marekani ikitarajiwa kufumuka mwaka 2012.

Taarifa hizo zimeweka msisistizo kwamba kila baada ya miaka 750 000 dunia imekuwa ikihama kutoka umbali wa jua ambako hupata sumaku ya kujihimili na kwamba mpaka sasa imeshatoka zaidi ya umbali wa kilometa 30, jambo linalotajwa kuwa ni la hatari zaidi.

Habari ya mwisho wa dunia zimevuta hisia za watu wengi na kuleta mijadala mirefu baina ya wanaoamini na wasioamini, ambapo picha mbalimbali za namna tukio hilo litakavyokuwa zimeongezeka kwenye mitandao ya intaneti.

Katika hali inayoonesha kuwa mjadala ni mkubwa miongoni mwa jamii kampuni moja nchini Marekani imetengeneza filamu iitwayo 2012 ambayo inaonyesha namna dunia itakavyoteketea. Habari zaidi kuhusu tishio hili zinapatikana zaidi kwenye mitandao ya Intaneti.
Wakati huo huo, imani ya Kiislam nayo inaonekana kugusana na utabiri pale maandiko yake yanaposema kuwa, kiyama kitakuwa siku ya Ijumaa huku kalenda yan kizungu inaoensha Desemba 21, 2012 itakuwa Ijumaa.
Lakini maandiko wa Kiyunani ambayo ndiyo yametumika kuandaa Biblia Takatifu, yanaonekana kupingana na utabiri huo pale Masiah alipojibu swali la siku gani itakuwa mwisho wa dunia.
Masiah alijibu, si yeye, hata malaika walioko mbinguni hawajui mwisho wa dunia utakuwa lini, ila Mungu pekee.
Hii si mara ya kwanza kwa wanasayansi na watabiri kudai kujua mwisho wa dunia, mwaka 1982 walisema ungekuwa mwisho wa dunia kwa sababu sayari zingejipanga mstari mmoja na kugongana.
Tukio hilo lilitokea kweli, lakini dunia iliendelea kusimama katika muhimili wake huku wanasayansi hao wakidai kumbe ni tukio lilojiri kila baada ya miaka 500.
Baada ya hapo, wakadai mwaka 2000 ungekuwa mwisho wa dunia (Y2K) kwa vile programu zote za maisha ya wanadamu zingeishia mwaka 1999, hata Kompyuta zingegota hapo, lakini tukio hilo nalo halikutokea, dunia ikaendelea kuwepo.

2 comments:

  1. HAKUNA AJUATE MWISHO WA DUNIA ISIPOKUWA MUNGU PEKE YAKE. MANENO YANAYOSAMBAZWA KWENYE INTERNET NI MAWAZO YA BINADAMU AMBAYO YANA USHETANI NDANI YAKE. ALIYEUMBA MBINGU NA NCHI NDIYE MWENYE MAMLAKA PEKE YAKE YA KUJUA MWISHO WA DUNIA. HIVYO WATU WAACHE KUZUNGUMZIA MASWALA YASIYOWAHUSU NA WAJITAHIDI KUKESHA KILA WAKATI KWA MAANA HAKUNA ANAYEJUA SIKU WALA SAA. WANAPOTEZA MUDA WAO WA KUJIANDAA NA KUKAA WANASAMBAZA MAMBO YA UONGO. TUSIPOTEZE MUDA BURE HAKUNA ANAYEJUA LOLOTE KUHUSU MWSHO WA DUNIA HATA WALE WATAKATIFU WALIOKO MBINGUNI HAWAJUI HILO.

    ReplyDelete
  2. yes mungu pekee asema mimi ndiye wewe nani wataka kujuwa sili za MUNGU

    ReplyDelete