Wednesday, May 18, 2011

Kipato kidogo na jinsi ya kukitumia kwa mafanikio



Watu wengi husindwa kubana matumizi kutokana na kukosa elimu ya jinsi ya kutumia pesa. Baadhi wamesoma na wengine wanaendelea kusoma masomo mbalimbali yanayohusu pesa na wanahitimu vizuri, lakini wanapokuja katika uhalisia wa maisha wanajikuta wanafeli vibaya kutokana na kutoutambua umuhimu wa kuwa na nidhamu ya pesa.
Msomaji wangu nikupe dondoo kadhaa ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaweza kukusaidia katika kubana matumizi na hatimaye hata kama kipato chako ni kidogo, kikakidhi mahitaji yako muhimu na pia kukawepo na ziada.
Usipendelee kukopa
Kuna watu wengi sana wanaishi kwa kukopa kopa vitu madukani na kwa watu. Mtindo huu ni mbaya sana kwa ukadiriaji wa matumizi, kwani haumtii uchungu mkopaji hadi pale atakapokuwa analipa. Mara nyingi ukopaji huongeza gharama, hivyo inashauriwa ukiwa na 5,000 itumie hiyo, bila kutafuta ziada kwenye deni.
Kuwa na bajeti ndogo
Katika maisha pendelea kupanga bajeti yako kwa mafungu madogo madogo hasa ya wiki. Usivuke mipango hiyo kwa kutumia bajeti ya wiki inayofuata.
Usitembee na pesa nyingi
Baadhi ya watu wanapenda kutembea mitaani huku wakiwa na pesa nyingi mifukoni. Fahamu kuwa kutembea na pesa usizozipangia bajeti utajikuta unashawishiwa kuzitumia bila mpango.
Hata hivyo, unashauriwa kujenga tabia ya kukaa nyumbani na familia yako na kama utatoka siku za mwisho wa wiki basi weka bajeti ya kiasi ambacho utakitumia. Kitendo cha kutoka huku ukiwa na fedha nyingi kwenye pochi lako ni kujishawishi kufanya matanuzi yasio na msingi.
Epuka kununua vitu kwa rejareja!
Unapopata mshaara wako au unapofikiria kuhusu matumizi ya nyumbani kwako pendelea sana kununua vitu kwa jumla ambavyo utavitumia kwa mwezi mzima. Epuka kununua vipimo vidogo vidogo kwani vinaumiza na kuvuruga bajeti.

Pika chakula nyumbani kwako
Watu wengi hasa vijana wanapenda sana kula kwenye migahawa na hotelini. Ulaji huu ni ghali, hivyo inashauriwa kila mtu ajipikie chakula chake nyumbani. Hii itamsaidia kutumia pesa kidogo katika suala la chakula.

Ifundishe familia nidhamu ya pesa
Kuna watu hawawafundishi watoto na wake zao nidhamu ya matumizi ya pesa. Mume/mke asinunue vitu ambavyo familioa haikuzitengea bajeti na asiwepo mtumia hovyo vitu vilivyonunuliwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Akiba na mipango ni muhimu
Familia lazima ijiwekee akiba benki. Utunzaji wa pesa nyumbani si wa salama na mara nyingi hushawishi matumizi. Aidha unapoweka feda benki ziwekee malengo amambo utakuwa ukiyatimiza taratibu si mpaka pesa hizo ziwe nyini.

Kuwa na familia ndogo
Ingawa ni hali halisi ya maisha ya kiafrika kwa familia moja kuwa na watu wengi lakini inashauriwa kwamba, ili kupata ziada ya kipato lazima familia iwe ndogo, vinginevyo mshahara wote unaweza kutumika kwa chakula tu. La kama familia itakuwa ni kubwa basi kila mmoja afanye kazi ili uwepo usaidianaji wa kuendesha familia.

4 comments: