Wednesday, June 23, 2010

Nashindwa kusoma kwa maumivu ya kuachwa




Naitwa Rehema. Tatizo langu kubwa Anko Rich ni kuachwa. Nilikuwa na mchumba ambaye tulipanga kuoana, baada ya mimi kumaliza masoma yangu. Lakini kabla sijawa naye kimapenzi nilikuwa na mvulana mwingine.
Wiki chache ziliopita nikiwa chuo, yule mpenzi wangu wa zamani alikuja tukaenda kukaa naye kwenye mgahawa. Tukiwa huko kuna mtu alimpigia simu mchumba wangu akamwambia aje anifumanie.

Haukupita muda akafika pale tulipokuwa tumekaa. Kusema kweli hatukuwa na mazungumzo ya mapenzi ila tulizungumzia maisha kwani tulikuwa tumepotezana muda mwingi. Mchumba wangu alipofika akafoka na tangu siku hiyo akawaambia ndugu zangu kuwa kaniacha na hataki niwe naye tena. Nimejitahidi kumbembeleza hataki na kibaya zaidi hapokei simu yangu. Nimechanganyikiwa, nifanyeje maana hata masomo siyapandi tena, kutwa nashinda nalia.

Njia ambayo unaweza kuitumia ni kumtafua rafiki au ndugu kipenzi wa mchumba wako, umwelezee kilichotokea na ikiwezekana umtume akakuombee msahamaha kwa mchumba wako. Kuumizwa na tatizo bila kulitafutia ufumbuzi ni sawa na kulikuza. Tambua kwamba utakapokuwa ukitafuta ufumbuzi wa tatizo, sumu ya maumivu itakuwa ikinyonywa hii haijalishi kama utasamehewa au la!

Lakini pia unaweza kuwatuma wazee wakaenda kwao na huyo mchumba wako wakaombe kukutana naye ili kutafuta suluhu. Nina imani atakuelewa, asipokuelewa, basi ujue alishakuacha zamani kabla ya kukufumania huko na kwamba alikuwa akitafuta sababu tu!

Utafiti unaonesha kuwa wapenzi wanaoachwa au kuachana hawafikii hatua hiyo ghafla isipokuwa mipango ya siku nyingi. Unaweza kukuta mtu ameshamchukia mwenzake kwa sababu na kasoro kadhaa kwa muda mrefu na akabaki anatafuta sababu tu ya kumuacha, hivyo akiipata mtu wa namna hiyo huwa hayuko radhi kuombwa msamaha.
Nakuomba uketi chini ufikirie maisha yako, kwani ukiharibu masomo yako utakuwa umepata hasara kubwa. Kupenda kupo siku zote,, upendo haujawahi kupotea kwa wanadamu na vya kupenda vipo vingi.
Kudhani kwamba huyu akikuacha hakuna wa kumpenda zaidi yake ni kujidanganya., Kumbuka zamani ulikuwa unapenda samaki na viazi vya kwenu lakini leo vimekukinai na unapenda mkate. Jiulize mara mbili, tangu umezaliwa ulipenda vingapi na leo huvipendi tena. Hata kwa huyo aliyekuacha anaweza kukutenda lakini baadaye ukampata mingine wa kuziba nafasi yake.

No comments:

Post a Comment